Most Popular

DUA NA NYIRADI MBALIMBALI KABLA YA KULALA

17.8.2016

Nyiradi za kulala

Alikuwa Mtume صلى الله عليه وسلم akienda kulala usiku anakusanya viganja vyake kisha akivipuliza na akivisomea Suratul-Ikhlaasw, na Suratul-Falaq, na Suratun-Naas, kisha akipangusa kwa hivyo viganja vyake kiasi anachoweza katika mwili wake, akianza kichwani na usoni na mbele . (akifanya hivyo mara tatu)


1.

Mtume صلى الله عليه وسلم amesema : “Ukienda kulala soma Ayatul-Kursiy mpaka uimalize kwani Allaah ataendelea kukuhifadhi wala hakukaribii Shaytwaan mpaka asubuhi” (اللّهُ لا إلهَ إلاّ هُـوَ الـحَيُّ القَيّـومُ لا تَأْخُـذُهُ سِنَـةٌ وَلا نَـوْمٌ …) (Suratul-Baqarah -255)



2.

Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم “Anayesoma aya mbili za mwisho wa Suratul-Baqarah usiku zinamtosheleza" (آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ كُلٌّ آمَنَ بِاللّهِ وَمَلآئِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لاَ نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ وَقَالُواْ سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ) ( لاَ يُكَلِّفُ اللّهُ نَفْسًا إِلاَّ وُسْعَهَا لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ رَبَّنَا لاَ تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا رَبَّنَا وَلاَ تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا رَبَّنَا وَلاَ تُحَمِّلْنَا مَا لاَ طَاقَةَ لَنَا بِهِ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَآ أَنتَ مَوْلاَنَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِين) (Suratul-Baqarah 285-286)



3.

Mtume صلى الله عليه وسلم pia amesema: “Akiamka mmoja wenu kutoka usingizini kisha akarudi basi akikukute kitanda kwa shuka yake mara tatu na amtaje Allaah kwani hajui kilicho kuja baada yake. Na Akilala aseme: بِاسْمِكَ رَبِّـي وَضَعْـتُ جَنْـبي ، وَبِكَ أَرْفَعُـه، فَإِن أَمْسَـكْتَ نَفْسـي فارْحَـمْها ، وَإِنْ أَرْسَلْتَـها فاحْفَظْـها بِمـا تَحْفَـظُ بِه عِبـادَكَ الصّـالِحـين “Kwa jina lako Mola wangu, nimeweka ubavu wangu na kwa ajili yako nitaunyanyua, na ukiizuia (ukiichukua) roho yangu basi irehemu na ukiirudisha basi ihifadhi kwa kile unacho wahifadhi nacho waja wako wema.



4.

اللّهُـمَّ إِنَّـكَ خَلَـقْتَ نَفْسـي وَأَنْـتَ تَوَفّـاهـا لَكَ ممَـاتـها وَمَحْـياها ، إِنْ أَحْيَيْـتَها فاحْفَظْـها ، وَإِنْ أَمَتَّـها فَاغْفِـرْ لَـها . اللّهُـمَّ إِنَّـي أَسْـأَلُـكَ العـافِـيَة “Ee Allaah hakika Wewe umeiumba nafsi yangu nawe utaiua, ni kwako uhai wa nafsi yangu na ufaji wake, ukiipa uhai basi ihifadhi, na ukiifisha (ukiiua) basi isamehe. Ee Allaah hakika mimi nakuomba afya njema.



5.

Alikuwa Mtume صلى الله عليه وسلم akitaka kulala anaweka mkono wake wa kulia chini ya shavu lake kisha anasema: اللّهُـمَّ قِنـي عَذابَـكَ يَـوْمَ تَبْـعَثُ عِبـادَك “Ee Allaah nikinge mimi kwa adhabu yako siku utakayo wafufua waja wako.” (mara tatu)



6.

بِاسْـمِكَ اللّهُـمَّ أَمـوتُ وَأَحْـيا “Kwa jina lako Ee Allaah ninakufa na ninakuwa hai.”



7.

Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: “Hivi niwafahamishe juu ya kitu ambacho ni bora zaidi kuliko mtumishi wakati munapolala; Msabihini Allaah mara thelathini na tatu, kisha msifuni Allaah mara thelathini na tatu, na kisha mtukuzeni mara thelathini na tatu kwani kufanya hivi ni bora kwenu kuliko mtumishi” سُبْـحانَ الله “Ametakasika Allaah" (Mara thelathini na tatu) أَلْحَمْدُ لِلَّه “Sifa njema zote ni za Allaah" (Mara thelathini na tatu) اللَّه أكْبَرُ “Allaah Mkubwa” (Mara thelathini na tatu)



8.

اللّهُـمَّ رَبَّ السّمـواتِ السَّبْـعِ وَرَبَّ العَـرْشِ العَظـيم ، رَبَّنـا وَرَبَّ كُـلِّ شَـيء ، فالِـقَ الحَـبِّ وَالنَّـوى ، وَمُـنَزِّلَ التَّـوْراةِ وَالإنْجـيل ، والفُـرْقان ، أَعـوذُ بِـكَ مِن شَـرِّ كُـلِّ شَـيءٍ أَنْـتَ آخِـذٌ بِنـاصِـيَتِه . اللّهُـمَّ أَنْـتَ الأوَّلُ فَلَـيسَ قَبْـلَكَ شَيء ، وَأَنْـتَ الآخِـرُفَلَـيسَ بَعْـدَكَ شَيء ، وَأَنْـتَ الظّـاهِـرُفَلَـيْسَ فَـوْقَـكَ شَيء ، وَأَنْـتَ الْبـاطِـنُ فَلَـيْسَ دونَـكَ شَيء ، اقـْضِ عَنّـا الـدَّيْـنَ وَأَغْـنِنـا مِنَ الفَـقْر “Ee Allaah Mola wa mbingu saba na Mola wa arshi tukufu, Mola wetu na Mola wa kila kitu Mwenye kuichanua tembe ya mbegu na kokwa na alieteremsha Tawraat na Injiyl na Qur-aan, najikinga kwako kutokana na shari ya kila kitu. Wewe ndie mwenye kukamata utosi wake. Ee Allaah, Wewe ndie wa Mwanzo hakuna kabla yako kitu, nawe ndie wa Mwisho, hakuna baada yako kitu, na wewe ndiye uliewazi, hakuna juu yako kitu chochote na Wewe ndiye uliyefichika hakuna kilichojificha chini yako. Tulipie madeni yetu na utuepushe na ufakiri.



9.

الـحَمْدُ للهِ الَّذي أَطْـعَمَنا وَسَقـانا، وَكَفـانا، وَآوانا، فَكَـمْ مِمَّـنْ لا كـافِيَ لَـهُ وَلا مُـؤْوي “Sifa njema ni za Allaah ambaye ametulisha na ametunywesha na akatutosheleza na akatuhifadhi, ni wangapi ambao hawana wa kuwatosheleza wala wa kuwahifadhi.



10.

اللّهُـمَّ عالِـمَ الغَـيبِ وَالشّـهادةِ فاطِـرَ السّماواتِ وَالأرْضِ رَبَّ كُـلِّ شَـيءٍ وَمَليـكَه، أَشْهـدُ أَنْ لا إِلـهَ إِلاّ أَنْت، أَعـوذُ بِكَ مِن شَـرِّ نَفْسـي، وَمِن شَـرِّ الشَّيْـطانِ وَشِـرْكِه، وَأَنْ أَقْتَـرِفَ عَلـى نَفْسـي سوءاً أَوْ أَجُـرَّهُ إِلـى مُسْـلِم . “Ee Allaah mjuzi wa yaliyojificha na yaliyo wazi, Muumba wa mbingu na ardhi, mola wa kila kitu na Mfalme wake, nakiri kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Wewe, najilinda kwako na shari ya nafsi yangu na shari ya Shaytwaan na shirki yake na kujichumia uovu kwa nafsi yangu au kumletea Muislamu.



11.

Ukitaka kulala tawadha wudhuu kama wa Swalah kisha lalia ubavu wako wa kulia kisha sema: اللّهُـمَّ أَسْـلَمْتُ نَفْـسي إِلَـيْكَ، وَفَوَّضْـتُ أَمْـري إِلَـيْكَ، وَوَجَّـهْتُ وَجْـهي إِلَـيْكَ، وَأَلْـجَـاْتُ ظَهـري إِلَـيْكَ، رَغْبَـةً وَرَهْـبَةً إِلَـيْكَ، لا مَلْجَـأَ وَلا مَنْـجـا مِنْـكَ إِلاّ إِلَـيْكَ، آمَنْـتُ بِكِتـابِكَ الّـذي أَنْزَلْـتَ وَبِنَبِـيِّـكَ الّـذي أَرْسَلْـت “Ee Allaah nimeisalimisha nafsi yangu kwako, na nimekuachia mambo yangu Wewe na nime uelekeza uso wangu kwako na nimeutegemeza mgongo wangu kwako, kwa matajarajio na kwa kukuogopa, hapana sehemu ya kukimbilia wala ya kujiokoa ila kwako, nimekiamini kitabu chako ulicho kiteremsha na Mtume wako uliyemtuma.” Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم:"kwa mwenye kusema haya kisha ukifa utakuwa umekufa katika Uislamu.




Posted By: MJOMBA ZECODER

DUA NA NYIRADI MBALIMBALI KABLA YA KULALA

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© HABARI KUHUSU WAISLAMU All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger