Most Popular

NYINGINEZO

    26.08.2016

Waislamu Marekani waendeleza kampeni za kuutangaza vizuri Uislamu

Add caption
 Wanachuo Waislamu wa Chuo Kikuu cha jimbo la Wisconsin nchini Marekani wameanzisha kampeni ya kugawa chakula kwa watu wasio na makazi wa mji wa Madison ili kuwapa fursa ya kuujua Uislamu na kuuliza maswali kuhusiana na dini hiyo ya Mwenyezi MunguENDELEA

 

26.08.2016

Ndugu watatu Waislamu wateremshwa kwenye ndege kwa kutuhumiwa kuwa wanachama wa Daesh

 

 Ndugu watatu Waislamu raia wa Uingereza wamefikwa na mkasa wa kuteremshwa kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa London na kuhojiwa kwa muda wa saa nzima baada ya abiria wenzao kuwatuhumu kuwa ni wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh.ENDELEA

26.08.2016

Mwanamke aliyekataa kuvua Hijabu afukuzwa kazi Ujerumaini

Mwanamke mmoja aliyekuwa masomoni kwenye mji wa Luckenwalde nchini Ujerumani amefukuzwa kazi kwa kukataa kuvua Hijabu.
Meya wa mji wa Luckenwalde, Elisabeth Herzog-von der Heide
Gazeti la Daily Mail limeripoti habari hiyo na kusema kuwa, mwanamke huyo Muislamu mwenye asili ya Palestina, alifukuzwa kazi jana Alkhamisi katika siku yake ya kwanza kuripoti kazini katika manispaa ya Luckenwalde, mkoani Brandenburg, Ujerumani.ENDELEA

 

 

 22.08.2016

IRANI:

Ayatullah Khamenei:Msikiti ni kituo cha kuandaa mazingira kwa ajili ya kuleta ustaarabu wa Kiislamu.

 Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, msikiti unapaswa kuwa kituo cha kumjenga mwanadamu kukabiliana na adui, kuujenga moyo kimaanawi na kidunia, kuongeza muono na kuandaa mazingira kwa ajili ya kuleta ustaarabu wa Kiislamu.

   Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akiendelea kuzungumzia umuhimu wa msikiti amesema kuwa, katika historia ya Uislamu, msikiti ulikuwa ni makao makuu ya mashauriano, ushirikiano na sehemu ya kuchukua maamuzi kuhusiana na masuala muhimu ya kijamiii, kisiasa na kijeshi.ENDELEA

 

21.08.2016

Wanawake Waislamu kutoka Iran, Misri washinda medali katika Taekwondo Olimpiki Rio

  Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Misri zimepata medali zao za kwanza za mashindano ya taekwondo ya wanawake katika michezo ya Olimpiki ya Rio, 2016.

 Kwa mujibu wa mwandishi wetu, wanawake wachanga kutoka nchi za Kiislamu ni nguvu ibuka katika taekwondo na hilo limebainika kufuatia mafanikia makubwa waliyopata katika michezo ya Olimpiki ya Rio di Janeiro nchini Brazil mwaka huu wa 2016.ENDELEA

19.08.2016

Waislamu waandamana Marekani kulaani udhalilishwaji wa wanawake wawili wa Kiislamu.

 Waislamu wa eneo la Rogers Park mjini Chicago nchini Marekani wamefanya maandamano kulaani vitendo vya udhalilishaji walivyofanyiwa wanawake wawili wa Kiislamu mjini hapo.

Habari kutoka mjini Chicago zimearifu kwamba wakazi wa eneo hilo wakiwemo Waislamu na wasio Waislamu, sambamba na kumiminika mabarabarani kulaani kitendo hicho, wameitaka polisi ikitaje kitendo hicho kuwa ni kosa la kuchukiza sanjari na kuanzisha uchunguzi juu yake. Aidha waandamanaji hao mbali na kupiga nara dhidi ya vitendo vya udhalilishaji wanavyofanyiwa Waislamu, wameonyesha machungu yao kwa ajili ya wanawake hao wa Kiislamu.ENDELEA

 

19.08.2016

Utafiti: Uislamu ndiyo dini inayokuwa kwa kasi zaidi duniani

 

 Utafiti uliofanywa na kituo cha utafiti cha Pew Research Center cha Marekani umeonyesha kuwa, Uislamu utasalia kuwa dini yenye kukuwa kwa kasi zaidi duniani katika kipindi cha miongo kadhaa ijayo.

Shirika la Bloomberg limeripoti kuwa, utafiti wa kituo cha Pew chenye makao makuu yake mjini Washington umebainisha kuwa, idadi kubwa ya watu wanavutiwa na Uislamu kutokana na mafundisho yake, haswa kuhusu miamala na bishara za halali. Utafiti huo umesema kuwa, idadi kubwa ya watu wanavutiwa na namna Uislamu unavyofundisha juu ya kupata kipato cha halali na kujihusisha na biashara na uwekezaji unaofuata sheria na mafundisho ya Qurani tukufu.ENDELEA

                  

 19.08.2016

Waziri Mkuu wa Ufaransa aunga mkono marufuku ya 'burqini

Burqini
Waziri Mkuu wa Ufaransa ameunga mkono hatua ya mameya wa miji minne nchini humo kupiga marufuku vazi la stara la kuogelea linalovaliwa na wanawake wa Kiislamu linalofahamika kama 'burqini'.

Manuel Valls amesema vazi hilo haliendani na thamani, utamaduni na desturi ya Wafaransa na hivyo ni sawa kwa wanawake wa Kiislamu kutoruhusiwa kulivaa wanapoenda kuogelea kwenye fukwe za umma.ENDELEA

 

 19.08.2016   

Wafuasi 418 wa Ikhwanul Muslimin wahukumiwa adhabu kali na mahakama ya kijeshi ya Misri.

Mahakama ya kijeshi ya Misri imetoa hukumu ya vifungo vya kuanzia miaka miwili hadi maisha jela kwa watu 418 ambao ni wanachama na wafuasi wa harakati ya Kiislamu ya Ikhwanul Muslimin.

             

Mahakama hiyo imetoa hukumu kwa watu 350 bila ya wenyewe kuwepo mahakamani za kuanzia miaka 25 hadi kifungo cha maisha jela. Washtakiwa 68 waliokuwepo mahakamani wamehukumiwa vifungo vya kati ya miaka miwili hadi kumi jela.ENDELEA

       

18.08.2016

Wanariadha waonyesha nguvu za Uislamu katika Olimpiki Rio

 

Wanariadha watatu Waislamu wameonyesha nguvu na taswira nzuri ya Uislamu katika michezo ya Olimpiki ya Rio, 2016.

Kwa mujibu wa mwandishi wa chanzo chetu cha habari, jarida la Time limechapisha taswira za baadhi ya wanariadha Waislamu ambao wamepata medali katika michezo ya Olimpiki inayoendelea mjini Rio nchini Brazil. Pamoja na kuwepo chuki dhidi ya Uislamu, wanariadha Waislamu wamewasilisha taswira nzuri katika michezo ya RioENDELEA

 

 

 

 

  18.08.2016
Mashindano ya Qur’ani ya msimu wa joto yameanza mjini Bidiya nchini Oman.ENDELEA

 

18.08.2016

Mwanamke wa kwanza Mwislamu kuchaguliwa kugombea ubunge Minnesota, Marekani

Mwanamke Mwislamu Mmarekani, Ilhan Omar ameweka historia kwa kuchaguliwa kugombea kiti katika Bunge la Wilaya ya 60B jimbo la Minnesota nchini MarekaniENDELEA

 

 

 

MAREKANI:IMAMU NA MSAIDIZI WAKE WAUAWA


Duru za habari zinaarifu kuwa, Imam Alala Uddin Akongi wa Msikiti wa Jamia wa Al-Furqan na msaidizi wake aliyetambulika kama Thara Uddin waliuawa kwa kufyatuliwa risasi jana Jumamosi walipokuwa wakitoka kuswali swala ya Adhuhuri katika barabara ya Ozone, mji wa Borough of Queens jimboni New York.

IMAMU MAULAMA AKONJEE


Imamu Maulama Akonjee, 55, aliwasili Newyork miaka miwili iliyopita kutoka Bangladesh.
Baraza la Mahusiano ya Kiislamu na Marekani limelaani mauaji hayo na kusema kuwa wawili hao mbali na kuwa viongozi wa kidini, walikuwa viongozi wa kijamii katika mji huo. Haya yanajiri wiki moja baada ya wanajeshi waliostaafu katika jimbo la Texas nchini Marekani kutishia kuwakata vichwa kwa mapanga Waislamu watakaoenda kutekeleza ibada ya swala katika Msikiti wa Al-Sahaabah mjini Wataunga jimboni hapo. Alia Salem, Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Mahusiano ya Kiislamu la Marekani, CAIR, katika eneo la Dallas sambamba na kulaani kitendo hicho, alisema baraza hilo limekuwa likipokea malalamiko kutoka kwa wasimamizi wa msikiti huo ambao wamekuwa wakitishiwa maisha kwa njia ya simu na watu wasiojulikana..


Watu wa asili ya Bangladesh mjini New York wamuomboleza Imam Akonjee


Ikumbukwe kuwa, katika miezi ya hivi karibuni vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu vimeongezeka mno nchini Marekani na barani Ulaya. Hivi karibuni Mkuu wa Baraza la Waislamu nchini Ujerumani (ZMD) alisema kuwa, kuna wasiwasi wa kuongezeka vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu katika nchi hiyo ya bara Ulaya. Pamoja na kuwepo propaganda chafu dhidi ya Uislamu lakini idadi ya watu wanaosilimu na kuingia katika dini hii tukufu imekuwa ikiongezeka kwa kasi mno katika ulimwengu wa Magharibi.


Posted By: MJOMBA ZECODER

NYINGINEZO

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© HABARI KUHUSU WAISLAMU All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger