Most Popular

Mashindano ya Qur’ani yaanza Oman

 18.08.2016

Mashindano ya Qur’ani ya msimu wa joto yameanza mjini Bidiya nchini Oman.




Kwa mujibu wa mwandishi wa Chanzo chetu cha habari, mashindano hayo yatawashirikisha watu kutoka makundi yote ya umri hasa vijana na mabarobaro wapatao 300 ambapo kutakuwa na vitengo tafauti vya wanawake na wanaume.
Halikadhalika mashindano hayo yatawashirikisha raia wa kigeni waishio Oman na wanafunzi vya vyuo vikuu na wake nyumbani.


Mashindano hayo yatakuwa na kategoria za kuhifadhi Juzuu moja, Juzuu 15, Juzuu 20 na Sura al Kahf kwa kuzingatia misingi ya tajweed katika kusoma Qur’ani Tukufu.


Washindi watapata zawadi za fedha taslimu na cheti cha kushiriki.
Posted By: MJOMBA ZECODER

Mashindano ya Qur’ani yaanza Oman

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© HABARI KUHUSU WAISLAMU All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger