Mwanamke mmoja aliyekuwa masomoni kwenye mji wa Luckenwalde nchini Ujerumani amefukuzwa kazi kwa kukataa kuvua Hijabu.
Gazeti la Daily Mail limeripoti
habari hiyo na kusema kuwa, mwanamke huyo Muislamu mwenye asili ya
Palestina, alifukuzwa kazi jana Alkhamisi katika siku yake ya kwanza
kuripoti kazini katika manispaa ya Luckenwalde, mkoani Brandenburg,
Ujerumani.
![]() |
Meya wa mji wa Luckenwalde, Elisabeth Herzog-von der Heide |
Amedai kuwa, kuvaa vazi la Hijabu katika ofisi za meya wa mji huo, eti kutaiopotezea itibari ya kijamii ofisi yake.
Amedai pia kuwa, masuala ya kiitikadi hayapaswi kusababisha machafuko na wasiwasi katika jamii.
Hata hivyo hatua ya meya huyo
imelalamikiwa na baadhi ya idara za serikali pamoja na taasisi za
kijamii za Ujerumaini na kusema kuwa hatua hiyo ni kinyume cha sheria na
kuitaka manispaa ya mji huo ulioko umbali wa kilomita 70 kusini mwa
Benlin, iache ubaguzi wa kidini katika kuajiri wafanyakazi wake.
No comments:
Post a Comment