Mwanamke Mwislamu Mmarekani, Ilhan Omar ameweka historia kwa kuchaguliwa
kugombea kiti katika Bunge la Wilaya ya 60B jimbo la Minnesota nchini
Marekani.
Akizungumza baada ya matokeo ya uchaguzi huo wa mchujo wa Agosti 6,
Ilan Omar wa chama cha Democrat na mwenye asili ya Somalia alisema. "Leo
tumeandika historia. Leo ni mwanza wa mustakabali mpya wa wilaya yetu.”
Ilhan Omar mwenye umri wa miaka 33 alizaliwa Somalia kabla
ya kukimbilia Marekani kutokana na vita katika nchi yake.
Alipokimbia Somalia awali aliishi kwa muda wa miaka mine
katika kambi ya wakimbizi nchini Kenya kabla ya kuelekea Marekani katika eneo
lenye Wasomali wengi la Cedar-Riverside ambapo aliishi kwa miongo miwili na sasa
ni mkurugenzi wa Jumuiya ya Kuwaleta Pamoja Wanawake.
Omar amemshukuru baba yake, mume na watoto wake pamoja na
hayati babu yake kwa kumfundihsa kuhusu demokrasia.
Mwezi Novembe Omar atachuana na Abdimali Askar wa chama cha
Republican katika uchaguzi wa kuwakilisha eneo hilo katika bunge la kieneo.
No comments:
Post a Comment