Most Popular

Ndugu watatu Waislamu wateremshwa kwenye ndege kwa kutuhumiwa kuwa wanachama wa Daesh

Ndugu watatu Waislamu raia wa Uingereza wamefikwa na mkasa wa kuteremshwa kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa London na kuhojiwa kwa muda wa saa nzima baada ya abiria wenzao kuwatuhumu kuwa ni wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh.
 Sakina Dharas mwenye umri wa miaka 24, ndugu yake Maryam mwenye umri wa miaka 19 na ndugu yao wa kiume Ali mwenye umri wa miaka 21 walikuwa wakisafiri wiki iliyopita na ndege ya EasyJet kutoka uwanja wa ndege wa Stansted, London kueleka mji wa Naples nchini Italia

Ndege waliyokuwa wakisafiria Sakina na ndugu zake

Sakina amevieleza vyombo vya habari kuwa wakati ndege ilipokuwa inakaribia kuruka mhudumu mmoja wa ndege hiyo aliwaamuru wateremke na kuwasindikiza hadi kwenye ngazi ya uwanja wa ndege ambako walikabidhiwa kwa askari polisi wenye silaha na afisa wa shirika la ujasusi la Uingereza MI5 na kusailiwa kwa muda wa saa moja.

Sakina, ambaye ni Mfamasia amesema walielezwa kuwa abiria mmoja ndani ya ndege alikuwa amedai kwamba wao ni wanachama wa Daesh (ISIS) kwa sababu aliwaona wakiangalia simu zao za mkononi zikiwa na maandishi ya Kiarabu au maneno yasomekayo "Hamdu ni za Allah".
Kwa mujibu wa msichana huyo, yeye na ndugu zake hata hawazungumzi Kiarabu na kwamba asili yao wao ni India.

Amesema kitu pekee cha Kiarabu kilichomo kwenye simu yake ni programu ya aya za Qur'ani, lakini hakuwa ameifungua programu hiyo kwa muda wote alipokuwa uwanja wa ndege kabla ya safari.
Kwa mujibu wa Sakina, wakati aliposailiwa alitakiwa watoe maelezo kuhusu muhuri mmoja mmoja uliogongwa kwenye pasi yake ya kusafiria pamoja na kuonyesha jumbe za karibuni za Whatsapp katika simu yake.

Maafisa wa kikosi cha kupambana na ugaidi cha Uingereza

Aidha waliulizwa kuhusu masuala binafsi yakiwemo ya anuani za nyumbani kwao, kazini, rekodi yao ya kujiunga na mitandao ya kijamii pamoja na kazi za wazazi wao.

Amesema tukio hilo la tuhuma za uongo liliwatia wahaka na tahayuri na kusisitiza kwamba wamekuwa waathiriwa wa vitendo vya ubaguzi
Posted By: MJOMBA ZECODER

Ndugu watatu Waislamu wateremshwa kwenye ndege kwa kutuhumiwa kuwa wanachama wa Daesh

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© HABARI KUHUSU WAISLAMU All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger