Most Popular

Waislamu Marekani waendeleza kampeni za kuutangaza vizuri Uislamu

Wanachuo Waislamu wa Chuo Kikuu cha jimbo la Wisconsin nchini Marekani wameanzisha kampeni ya kugawa chakula kwa watu wasio na makazi wa mji wa Madison ili kuwapa fursa ya kuujua Uislamu na kuuliza maswali kuhusiana na dini hiyo ya Mwenyezi Mungu


Shirika la habari la IQNA limemnukuu Bi Najiha Khan, mkuu wa taasisi ya wanachuo Waislamu akisema kuwa, kushirikiana na watu wa dini nyinginezo na kuwaonesha kuwa Waislamu nao ni sawa na watu wengine, ni mbinu nzuri ya kupambana na propaganda chafu zinazoenezwa dhidi ya Waislamu.

Amesema, kampeni hiyo inawapa fursa ya kujibu maswali mbalimbali yanayoulizwa kuhusu Uislamu na kuondoa hofu waliyo nayo baadhi ya watu kuhusiana na Waislamu.

Kuna jamii kubwa ya Waislamu nchini Marekani

Mwaka jana (2015) viongozi kadhaa wa kidni wasio Waislamu, walitembelea Kituo cha Kiislamu mjini Madison na kuwakabidhi viongozi wa kituo hicho tambara kubwa lenye saini 400  ili kuonesha kuwa, Waislamu nao ni raia wa Marekani.

Waliotia saini tambara hilo kubwa walisema kuwa, lengo la hatua yao hiyo ni kutangaza uungaji mkono wao kamili kwa Waislamu na kwamba wako tayari kutetea haki za Waislamu na kukabiliana vikali na kampeni za kueneza chuki dhidi ya Waislamu.
Posted By: MJOMBA ZECODER

Waislamu Marekani waendeleza kampeni za kuutangaza vizuri Uislamu

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© HABARI KUHUSU WAISLAMU All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger