Most Popular

Waislamu waandamana Marekani kulaani udhalilishwaji wa wanawake wawili wa Kiislamu


Waislamu wa eneo la Rogers Park mjini Chicago nchini Marekani wamefanya maandamano kulaani vitendo vya udhalilishaji walivyofanyiwa wanawake wawili wa Kiislamu mjini hapo.


Habari kutoka mjini Chicago zimearifu kwamba wakazi wa eneo hilo wakiwemo Waislamu na wasio Waislamu, sambamba na kumiminika mabarabarani kulaani kitendo hicho, wameitaka polisi ikitaje kitendo hicho kuwa ni kosa la kuchukiza sanjari na kuanzisha uchunguzi juu yake. Aidha waandamanaji hao mbali na kupiga nara dhidi ya vitendo vya udhalilishaji wanavyofanyiwa Waislamu, wameonyesha machungu yao kwa ajili ya wanawake hao wa Kiislamu

Mwanamke wa Kiislamu nchini Marekani

Aliya Amar, mmoja wa wasemaji wa mkusanyiko huo wa Waislamu amesema kuwa, karibu kila siku Waislamu nchini Marekani wamekuwa wakilengwa kwa vitendo vya kuchukiza vinavyotokana na chuki dhidi ya Uislamu na kwamba vitendo hivyo vimeshika kasi hasa baada ya kuanza kampeni za Donald Trump, mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican, na kutoa pendekezo la kuzuiliwa Waislamu wasiingie nchini Marekani


Wanawake wa Kiislamu na wasio Waislamu katika maandamano ya Chicago

Itakumbukwa kuwa mwezi uliopita wa Julai, Suzanne Damra, binti wa Kiislamu mwenye umri wa miaka 25 na mama yake mzazi walidhalilishwa kwa mara kadhaa na jirani yao. Aidha wiki iliyopita, jirani yao huyo mwenye chuki dhidi ya dini ya Kiislamu aliwashambulia kwa kuwapiga. Hii ni katika hali ambayo licha ya taarifa hiyo kuripotiwa kwa vyombo vya usalama, lakini bado polisi ya nchi hiyo haijachukua hatua yoyote ile.
Posted By: MJOMBA ZECODER

Waislamu waandamana Marekani kulaani udhalilishwaji wa wanawake wawili wa Kiislamu

No comments:

Post a Comment

About Us

Advertisment

Like Us

© HABARI KUHUSU WAISLAMU All rights reserved | Theme Designed by Mjomba Computers Published.. Blogger